عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«أَلْحِقُوا الفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَلِأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6737]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema:
"Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6737]
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kusimamia ugawaji wa mirathi wazigawe kwa wastahiki wake kwa mgao wa uadilifu wa kisheria kama alivyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, ataanza kwa kuwapa wale wenye fungu lililokadiriwa tayari kisheria, kulingana na mafungu yao katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni: Theluthi mbili, na theluthi moja, na sudusu (moja ya sita) na nusu, na robo, thumunu (moja ya nane), mali itakayobakia baada ya hapo, hiyo atapewa ndugu wa karibu na maiti katika wanaume, na ndugu hao huitwa aswaba (warithi wasio na mipaka).