+ -

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الدُّعَاءُ لاَ يُرَدُّ بَيْنَ الأَذَانِ وَالإِقَامَةِ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي] - [سنن الترمذي: 212]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake:
"Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 212]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai German Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية النيبالية الرومانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za wakati huu kwa ajili kuomba dua.
  2. Atakapojipamba muombaji kwa adabu za kuomba dua, na akatafuta mahala pake na nyakati zake bora, na akajiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, na akachukua tahahadhari ya kutotumbukia katika mambo yasiyofaa na yenye kutatiza, na akamdhania vizuri Mwenyezi Mungu: Basi ni rahisi sana kujibiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  3. Amesema Al-Munawi kuhusu kujibiwa dua: Yaani: Baada ya kukusanya sharti za dua na nguzo zake na adabu zake, ikiwa kitapelea kitu chochote basi asilaumu ila nafsi yake.
  4. Ni sunna kuomba dua: Ima zijibiwe haraka dua zake, au aepushiwe katika shari mfano wake, au atunziwe Akhera; na hii ni kulingana na hekima ya Mwenyezi Mungu na huruma yake.