+ -

عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال:
سَمِعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا يَعِظُ أَخَاهُ فِي الْحَيَاءِ، فَقَالَ: «الْحَيَاءُ مِنَ الْإِيمَانِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 36]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake kuhusu haya (Aibu) akasema: "Haya ni katika imani".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 36]

Ufafanuzi

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake aache kuwa na aibu sana! akambainishia kuwa haya ni katika imani, nakuwa huwa haiji ila kwa kheri.
Na haya ni tabia inayomsukuma mtu kufanya zuri na kuacha baya.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kinachokuzuia kufanya kheri hakiitwi kwa jina la haya, bali kitu hicho kinaitwa uoga na kushindwa na kufeli na hofu.
  2. Kumuonea haya Mwenyezi Mungu Mtukufu kunakuwa kwa kufanya maamrisho, na kuacha maharamisho.
  3. Kuwaonea haya viumbe kunakuwa kwa kuwaheshimu, na kumpa kila mtu nafasi yake, na kuyapuke yanayotia dosari siku zote.