عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «أكْثَرُ مَا يُدْخِلُ الْجَنَّةَ تَقْوَى اللَّهِ وَحُسْنُ الْخُلُقِ».
[حسن صحيح] - [رواه الترمذي]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie:"Vinavyowaingiza watu kwa wingi peponi ni uchamungu na tabia njema. ".
Ni nzuri na nisahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Katika hadithi kuna dalili ya ubora wa uchamungu, nakuwa ni sababu ya kuingia peponi, na vile vile katika ubora wa tabia njema, nakuwa mambo haya mawili (Uchamungu na tabia njema) ni katika sababu kubwa zinazomuingiza mja peponi.