عن سَمُرة بن جُنْدَب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «أحب الكلام إلى الله أربع لا يَضُرُّك بِأَيِّهِنَّ بدأت: سُبْحَانَ الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Samra bin Jundab Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Maneno yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni manne, haikudhuru kwa lolote utakaloanza nalo: Sub-haanallah (Ametakasika Mwenyezi Mungu) Al-hamdulillaah (Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu), Na, Laa ilaaha illa llaah, (Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu), Na Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu Mkubwa)".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Hadithi inaelezea ubora wa ibara hizi nne, nakuwa ni katika maneno yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kukusanya kwake mambo makubwa, nako ni kumtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na ni kumsifu kwa yote yanayolazimu kwake katika sifa za ukamilifu, na kumpwekesha kwa upweke wake na ukubwa, nakuwa ubora wake na kupata thawabu zake hakuna ulazima wa kuyapangilia kama yalivyokuja katika hadithi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuthibitishwa mapenzi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa yeye anapenda amali njema.
  2. Utukufu wa maneno haya manne kuliko mengine, nakuwa hayo yanapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu.
  3. Kuhimizwa juu ya kudumu na maneno haya manne, kwasababu mja anapojua mapenzi ya Mwenyezi Mungu katika kitu basi hudumu nacho na hukihifadhi.
  4. Wepesi wa sheria kwa watu "Haikudhuru kwa lolote kati ya hayo utakalo anza nalo".