عن جابر رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«أَفْضَلُ الذِّكْرِ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلهِ».
[حسن] - [رواه الترمذي والنسائي في الكبرى وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 3383]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema:
"Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah".
[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 3383]
Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dhikiri bora ni: "Laa ilaaha illa llaah" Na maana yake, hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa dua bora ni "Al-hamdulillaah"; Nayo inamaanisha kukiri kuwa mneemeshaji ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-, mwenye kustahiki sifa nzuri zilizokamilika.