عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ:
فَقَدْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيْلَةً مِنَ الْفِرَاشِ فَالْتَمَسْتُهُ فَوَقَعَتْ يَدِي عَلَى بَطْنِ قَدَمَيْهِ وَهُوَ فِي الْمَسْجِدِ وَهُمَا مَنْصُوبَتَانِ، وَهُوَ يَقُولُ: «اللهُمَّ أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقُوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ لَا أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 486]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 486]
Anasema Aisha radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nimelala pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamkosa wakati wa usiku, nikagusa kwa mkono wangu sehemu aliyokuwa akiswalia ndani ya chumba; ghafla nikamuona amesujudu na miguu yake ikiwa imesimamishwa, mara nikamsikia akisema:
"Ninajilinda" Na ninapitia "Katika radhi zako dhidi ya hasira zako" juu yangu au juu ya umma wangu, "na" ninaomba kinga "kwa salama yako" na msamaha wako mwingi "kutokana na adhabu zako", "na ninajilinda kwako kutokana nawe" na kwa sifa za uzuri wako kutokana na sifa za utukufu wako, kiasi kwamba hakuna awezaye kukinga dhidi yako ila wewe, hakuna pa kusalimika wala pa kujilinda kutokana na Mwenyezi Mungu ila kwake, "Siwezi kuzihesabu sifa zako" Sina uwezo wala siwezi kufikia kuzidhibiti na kuzihesabu kwa idadi kwa kushindwa kwangu kuzidhibiti kwa wingi neema zako na ihisani yako kama unavyostahiki, hata kama nikijitahidi katika hilo, "Wewe kama ulivyoisifia nafsi yako" wewe ndiye uliyeisifu dhati yako sifa zinazokustahiki, ni nani awezaye kutimiza haki ya sifa zako?!