عن ثَوْبَان -رضي الله عنه- قال: كان رسول الله -صلى الله عليه وسلم- إذا انْصَرف من صلاته اسْتَغْفَر ثلاثا، وقال: «اللهُمَّ أنت السَّلام ومِنك السَّلام، تَبَارَكْتَ يا ذا الجَلال والإكْرَام».
[صحيح.] - [رواه مسلم.]
المزيــد ...

Kutoka kwa Thauban -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehma na Amani ziwe juu yake- anapomaliza swala yake anataka msamaha mara tatu, na anasema: Allaahumma antas salaam, waminkas salaam, Tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam (Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni Amani, na Amani hutoka kwako, umetakasika Ewe mwenye Utukufu na ukarimu).
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

katika hadithi kuna ubainifu wa kupendeza kusema mwenye kuswali baada ya kumaliza swala: Namuomba Mwenyezi Mungu msamaha, Namuomba Mwenyezi Mungu msamaha, Namuomba Mwenyezi Mungu msamaha. Kisha asema dua hii: "Allaahumma antas salaam, waminkas salaam, Tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam". Na kuna dua zingine zilizokuja katika hadithi zingine katika yale yanayosemwa baada ya swala.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu
Kuonyesha Tarjama
1: Hapa kuna jibu kwa mwenye kusema kuwa: mwenye kuswali anatakiwa kutoa takbira (yaani kusema: Allaahu Akbar) baada ya swala.
2: Kuna uthibitisho wa jina la "Assalaam" (Amani) kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu- na sifa yake, yeye amesalimika na kila mapungufu na aibu, na yeye ndiye mgawaji wa Amani kwa waja wake kutokana na shari za dunia na Akhera.