+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ سَبَّحَ اللهَ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ، وَحَمِدَ اللهَ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ، وَكَبَّرَ اللهَ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ، فَتْلِكَ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ، وَقَالَ: تَمَامَ الْمِائَةِ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 597]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 597]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema baada ya kumalizika kwa swala za faradhi:
Mara thelathini na tatu (33): (Sub-haanallaah) Nako ni kumtakasa Mwenyezi Mungu dhidi ya mapungufu.
Na mara thelathini na tatu (33): (Alhamdulillaah) Nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa kamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
Na mara thelathini na tatu (33): (Allaahu Akbar) Nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkuu na Mtukufu kuliko kila kitu.
Na kwa kukamilisha idadi ya mia moja (100) "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku, walahul hamdu, wahuwa alaa kulli shai in-Qadiir" Na maana yake: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye pekee asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu ndiye alipwekeka kwa Ufalme kamilifu, na ndiye mwenye kustahiki kutukuzwa na sifa pamoja na mapenzi na kukwezwa pasina mwingine, nakuwa Yeye ni muweza hakuna kinachomshinda.
Yeyote atakayesema hivyo, dhambi zake zitafutwa na kusamehewa, hata zikiwa nyingi, kama povu jeupe litokalo juu ya bahari inapochafuka na kutibuka.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya dhikiri hizi kuzisema baada ya swala za faradhi.
  2. Dhikiri hizi ni sababu ya kusamehewa madhambi.
  3. Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehema zake na msamaha wake.
  4. Dhikiri hii ni sababu ya kusamehewa madhambi, na kinachokusudiwa hapa ni: kufutiwa madhambi madogo, ama madhambi makubwa hakuna kinachoweza kuyafuta isipokuwa toba.
Ziada