عَنْ أَبِي أُمَامَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ قَرَأَ آيَةَ الْكُرْسِيِّ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ لَمْ يَمْنَعْهُ مِنْ دُخُولِ الْجَنَّةِ إِلَّا أَنْ يَمُوتَ».
[صحيح] - [رواه النسائي في الكبرى] - [السنن الكبرى للنسائي: 9848]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".
[Sahihi] - - [السنن الكبرى للنسائي - 9848]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema kuwa mwenye kusoma Ayatul-Kursi baada ya kumalizika kwa swala ya faradhi, hakuna kitakachomzuia kuingia Peponi isipokuwa kifo; nayo iko katika Suratul Baqarah, Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu - hapana mungu isipokuwa Yeye, Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika elimu yake isipokuwa kwa kile akitakacho. Kuti chake cha enzi kimeenea mbingu na dunia, na wala halemewi na kuvilinda vyote viwili. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu." [Al-Baqara: 255]