Aina za kimatawi

Orodha ya Hadithi

Anasema: kila mwisho wa swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun ni'matu walahul Fadhlu, walahuth thanaaul hasan, Laa ilaaha Illa llaahu Mukhliswiina lahud diina walau karihal kaafiruun" Yaani: Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu, Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, Na hakuna tunayemuabudu ila yeye, ana neema na ana fadhila, na ana sifa njema, Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu tunamtakasia dini hata kama makafiri watachukia.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akisema kati ya sijida mbili: Allaahumma ghfirlii, warhamnii, wa aafinii, wahdinii. warzuqnii (Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya, na uniongoze, na uniruzuku)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehma na Amani ziwe juu yake- anapomaliza swala yake anataka msamaha mara tatu, na anasema: Allaahumma antas salaam, waminkas salaam, Tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam (Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni Amani, na Amani hutoka kwako, umetakasika Ewe mwenye Utukufu na ukarimu).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiomba: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na adhabu za kaburi, na adhabu ya moto, na mitihani ya uhai na kifo, na fitina za masihi dajali.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, Hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqaath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mu'adhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda, kisha ninakuusia ewe Mu'adhi, hakikisha usiache mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainniy alaa dhikirika -Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie mimi niweze kukutaja wewe, Washukurika- na kukushukuru, Wahusni ibaadatika -Na kuzifanya vizuri ibada zako.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Allaahumma inni Audhubiridhwaaka min sakhatwika, -Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, wabimuaafaatika min uquubatika,- Na kwa msamaha wako kutokana na adhabu zako-, Wa a'udhubika minka, -na ninajilinda kwako kwa ulinzi utokao kwako-, Laa uhswith thanaa 'alaika, -Siwezi kuzidhibiti shukurani zote juu yako, Anta kamaa athnaita a'laa nafsika, -Wewe kama ulivyojisifia nafsi yako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa