+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ:
مَا صَلَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلاَةً بَعْدَ أَنْ نَزَلَتْ عَلَيْهِ: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالفَتْحُ} [النصر: 1] إِلَّا يَقُولُ فِيهَا: «سُبْحَانَكَ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي». وعَنْها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ فِي رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ: «سُبْحَانَكَ اللهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللهُمَّ اغْفِرْ لِي» يَتَأَوَّلُ الْقُرْآنَ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4967]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4967]

Ufafanuzi

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipoteremshiwa juu yake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" Akaifasiri Qur'ani na akaanza kuitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: "Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi na umuombe msamaha", akawa akikithirisha kusema katika rukuu zake na sijida zake wakati wa swala: "Umetakasika" Na ni kukutakasa wewe dhidi ya kila mapungufu yale yasiyokufaa, "Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako" Kwa sifa nzuri kwako kwa ukamilifu wa dhati yako na sifa zako na matendo yako, "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe" na zifute kwangu dhambi zangu, na uziachilie mbali.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kupendeza kukithirisha dua hii katika rukuu na sijida.
  2. Kuomba msamaha mwisho wa umri kuna angalizo la kuhitimisha ibada zote namna hiyo, na hasa hasa swala kwa kuomba msamaha, ili azibe yale yaliyojitokeza ndani yake miongoni mwa mapungufu.
  3. Jambo zuri linalotumika kukubaliwa dua kupitia jambo hilo ni kutaja mazuri yake na sifa zake, na kumtakasa dhidi ya mapungufu na aibu.
  4. Fadhila ya kuomba msamaha, na kuutafuta katika kila hali.
  5. Ukamilifu wa utumwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutekeleza kwake amri ya Mwenyezi Mungu.
Ziada