عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما:
أَنَّ نَبِيَّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ عِنْدَ الْكَرْبِ: «لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ الْعَظِيمُ الْحَلِيمُ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَرَبُّ الْأَرْضِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2730]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema wakati wa matatizo: "Laa ilaaha illa llaahul a'dhwiimul haliim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbul A'rshil A'dhwiim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbu ssamaawaati warabbul A'rshil kariim" Tafsiri: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mpole, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa A'rshi tukufu, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa A'rshi takatifu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2730]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema wakati wa kuzidi kwa matatizo na huzuni kwake: "Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" Hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Mtukufu" wa cheo, Mtukufu wa shani, katika dhati yake na sifa zake na majina yake, "Mpole" asiyemharakisha mwenye kuasi kwa kumpa adhabu bali anaichelewesha, na anaweza kumsamehe pamoja nakuwa anauwezo wa kumuadhibu, yeye ndiye muweza Mtukufu juu ya kila kitu ni muweza. "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa Arshi tukufu" Muumba wa Arshi tukufu, "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa mbingu na ardhi" na muumba wa mbingu na ardhi, na muumba wa kila kitu ndani yake na mmiliki wake na mrekebishaji wake, na mwenye maamuzi ndani yake kwa namna yoyote aitakayo, "Mola wa Arshi karim" Muumba wa Arshi karim.