+ -

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ، وَلَا قَطِيعَةُ رَحِمٍ، إِلَّا أَعْطَاهُ اللهُ بِهَا إِحْدَى ثَلَاثٍ: إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ، وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا» قَالُوا: إِذنْ نُكْثِرُ، قَالَ: «اللهُ أَكْثَرُ».

[صحيح] - [رواه أحمد] - [مسند أحمد: 11133]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Ahmad] - [مسند أحمد - 11133]

Ufafanuzi

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa muislamu atakapomuomba Mwenyezi Mungu na akamuomba maombi ambayo si dhambi, kama kumuomba amrahisishie maasi na dhulma, na wala akawa hakuomba kukata udugu; kama kuwaombea dua mbaya watoto wake au ndugu zake wa karibu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa kwa dua yake hiyo moja kati ya mambo matatu: Ima amharakishie dua yake na ampe alichoomba. Na ima Mwenyezi Mungu amcheleweshee mpaka siku ya Kiyama kwa kumpa daraja za juu zaidi, na rehema na msamaha kutokana na madhambi. Na ima amkinge katika dunia na mabaya mfano wake kwa kiwango cha dua. Maswahaba wakasema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hivyo tukithirishe dua; ili tuweza kupata moja kati ya fadhila hizi? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni mengi na ni makubwa kuliko mnavyoviomba, kipawa chake hakimaliziki, na wala hakiishi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Dua ya muislamu hujibiwa hairejeshwi lakini kwa sharti zake na adabu zake; ndio maana inampasa mja akithirishe dua na wala asitake haraka ya kujibiwa.
  2. Kujibiwa dua hakufungamani na kupata kilichoombwa; kwani anaweza kumfutia madhambi kwa dua yake, au akamlimbikizia Akhera.
  3. Amesema bin Bazi: Kung'ang'ania, na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, na kutokata tamaa, hizi ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa, ni juu ya kila mtu kung'ang'ania katika dua, na awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na ajue kuwa yeye ni mwenye hekima na mjuzi, anaweza kuharakisha majibu kwa hekima, na anaweza kuyachelewesha kwa hekima, na anaweza kumpa muombaji kitu bora kuliko alichoomba.