عن عمرو بن شُعيب عن أبيه عن جدِّه قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم:
«مُرُوا أولادكمِ بالصلاةِ وهم أبناءُ سبعِ سِنينَ، واضرِبوهم عليها وهم أبناءُ عَشرٍ، وفرِّقوا بينهم في المَضاجِعِ».
[حسن] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 495]
المزيــد ...
Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 495]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa baba awaamrishe watoto wake wa kiume na wa kike kusali na umri wao ukiwa mikaa saba, na awafundishe wanayoyahitaji kwa ajili ya kuitekeleza. Na wakifikisha miaka kumi azidi kutilia mkazo, awapige wanapofanya uzembe, na awatenganishe katika vitanda.