+ -

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«إنَّ الرُّقَى والتَمائِمَ والتِّوَلَةَ شِرْكٌ».

[صحيح] - [رواه أبو داود وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 3883]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 3883]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vitu ambavyo kuvifanya kwake ni katika ushirikina; na miongoni mwavyo ni:
Cha kwanza: Makombe: Ni maneno ambayo watu wajinga huyatumia kama tiba yanayoambatana na ushirikina.
Cha pili: Vyenye kutundikwa ni kama hirizi na mfano wake: zinazotundikwa kwa watoto wadogo na wanyama na wengineo kwa ajili ya kuzuia kijicho.
Cha tatu: Limbwata: Ambalo hutengenezwa ili mmoja kati ya wanandoa amvute mwenzake kimapenzi.
Mambo haya yote ni katika ushirikina: Kwa sababu hii ni katika kukifanya kitu kuwa sababu, hali yakuwa si sababu ya kisheria iliyothibiti kwa ushahidi, wala si sababu inayoonekana wazi iliyothibiti kwa majaribio. Ama sababu za kisheria kama kusoma Qur'ani, au zenye kuonekana kama dawa zilizothibiti kwa majaribio, hizi zinafaa pamoja na kuamini kuwa hizi ni sababu tu, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuilinda tauhidi na itikadi dhidi ya yale yenye kuzibomoa.
  2. Uharamu wa kutumia makombe ya kishirikina na hirizi na limbwata.
  3. Mtu kuamini katika mambo matatu haya kuwa yenyewe ndiyo sababu: Hii ni shirki ndogo; Kwa sababu hii ni kuyafanya yasiyokuwa sababu kuwa ni sababu, ama akiitakidi kuwa yananufaisha na kudhuru yenyewe hii ni shirki kubwa.
  4. Tahadhari ya kufanya sababu za kishirikina na zilizoharamishwa.
  5. Kumeharamishwa makombe na kuwa ni katika shirki isipokuwa yale yatakayokuwa kisheria.
  6. Ni lazima moyo ufungamane na Mwenyezi Mungu peke yake, kwake ndio hutoka madhara na manufaa peke yake asiyekuwa na mshirika, hakuna aletaye kheri isipokuwa Allah na hakuna azuiaye shari isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  7. Ruqiya inayofaa ni ile iliyoambatana na sharti tatu: 1- Aitakidi kuwa ni sababu na wala haiwezi kunufaisha isipokuwa kwa idhini ya Allah. 2- Iwe kwa Qur'ani na majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake na dua za Mtume za kisheria. 3- Iwe kwa lugha inayofahamika, na wala isiambatane na matalasimu na mazingaombwe.