عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَتَى الْمَرِيضَ يَدْعُو لَهُ قَالَ: «أَذْهِبِ الْبَاسَ، رَبَّ النَّاسِ، وَاشْفِ أَنْتَ الشَّافِي، لَا شِفَاءَ إِلَّا شِفَاؤُكَ، شِفَاءً لَا يُغَادِرُ سَقَمًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2191]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2191]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomtembelea mgonjwa anamuombea dua kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu "Ondoa" ondosha "ugumu" na ukali wa maradhi, "Ewe Mola wa watu" na Muumba wao na Mlezi wao, "na ponya" maradhi haya "wewe" Mtukufu "Ndiye mponyaji" na ninaomba kupitia jina lako Mponyaji, "hakuna ponyo" linaloweza kupatikana kwa mgonjwa "isipokuwa ponyo lako" na afya yako, "ponyo" la moja kwa moja "lisiloacha" na kubakisha na kuacha "ugonjwa" na maradhi mengine.