+ -

عَن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2995]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2995]

Ufafanuzi

Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kupiga mwayo pale alipofungua kinywa chake kwa sababu ya uvivu au kujaa na mfano wake; kuwa aweke mkono wake juu ya kinywa chake ili akifunge kwa mkono; na hii ni kwa sababu Shetani huingia ndani yake anapokiacha wazi, kuweka mkono kunakuwa ni kizuizi cha kumzuia kuingia.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Atakapotaka mtu kupiga miayo anatakiwa auzuie kwa kadiri awezavyo, kwa kuuzuia mdomo wake, na aubakishe ukiwa umefungwa wala usifunguke, asipoweza kuubakisha mdomo wake ukiwa umefungwa basi aweke mkono wake juu ya mdomo wake, afunike kinywa chake kwa mkono wake.
  2. Kushikamana na adabu za kiislamu katika hali zote; kwa sababu ndio anwani ya ukamilifu na tabia njema.
  3. Kuchukua tahadhari ya kila mapitio ya Shetani kwa mwanadamu.