عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «أتدرون ما الغِيبَةُ؟»، قالوا: الله ورسوله أعلم، قال: «ذكرُك أخاك بما يكره»، قيل: أرأيت إن كان في أخي ما أقول؟ قال: «إن كان فيه ما تقول فقد اغْتَبْتَهُ، وإن لم يكن فقد بَهَتَّهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Je mnajua ni nini kusengenya?" wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema kwako ndugu yako kwa yale anayoyachukia" pakasemwa: Unasemaje yakiwa kwa ndugu yangu haya ninayoyasema? Akasema: "Akiwanayo hayo unayoyasema utakuwa umemsengenya, na akiwa hana basi utakuwa umemzulia uongo".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake maana halisi ya kusengenya, Nayo ni: kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyachukia, sawa sawa iwe ni katika sifa zake za kimaumbile au za kitabia hata kama sifa hizo atakuwa nazo, na ikiwa kama atakuwa hana sifa hizo basi utakuwa umekusanya pamoja na kusengenya sifa uongo na uzushi kwa mtu asiyekuwa nazo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kubainishwa maana ya kusengenya nikuwa ni kumsema kwako ndugu yako muislamu kwa yale anayoyachukia.
  2. Nikuwa kafiri si haramu kumsengenya katika yale ambayo ni ya kweli kwake, kwasababu hadithi imeishia kutaja usengenyaji kwa ndugu, na makusudio yake ni muislamu.
  3. Unapokuwa usengenyaji ni kumsema mtu kwa yale asiyokuwa nayo basi huo unakuwa ni uzushi.
  4. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na Amani ziwe juu yake kiasi ambacho anataja mambo kwa njia ya maswali.
  5. Uzuri wa adabu ya maswahaba wanapokuwa pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, pale waliposema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi.