+ -

عَن قُطْبَةَ بنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الأَخْلاَقِ وَالأَعْمَالِ وَالأَهْوَاءِ».

[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3591]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 3591]

Ufafanuzi

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga" Yani: Ninaomba ulinzi na ukaribu "kwako" na si kwa asiyekuwa wewe, "kutokana tabia mbovu" alizozikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "katika tabia" kama chuki na husuda na kiburi, "na" mabaya "katika matendo" kama kutukana na kushutumu, "na" yote "matamanio", ambayo nafsi inayatamani hali yakuwa yanakwenda kinyume na sheria.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa dua hii na kujibiwa kwake.
  2. Muumini anapupia kuepuka tabia mbaya na matendo maovu, na anachukua tahadhari ya kufuata matamanio na kutumbukia katika matamanio.
  3. Kugawanyika kwa tabia na matendo na matamanio katika maovu na mazuri.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama