عن عائشة رضي الله عنها قالت: سمعتُ من رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول في بيتي هذا:
«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1828]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema ndani ya nyumba yangu hii:
"Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1828]
Alimuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila atakayesimamia jambo katika mambo ya waislamu liwe dogo au kubwa, sawa sawa usimamizi huu uwe ni wa umma, au sekta binafsi, na akawaingizia tabu na hakuwahurumia, kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amlipe kutokana na matendo yake, kwa kumtia matatizo na yeye.
Nakuwa atakaye wahurumia na wakawafanyia wepesi, na akawarahisishia mambo yao basi Mwenyezi Mungu naye amuhurumie na ampe wepesi katika mambo yake.