+ -

قال سعد بن هشام بن عامر -عندما دخل على عائشة رضي الله عنها-:
يَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنْبِئِينِي عَنْ خُلُقِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: أَلَسْتَ تَقْرَأُ الْقُرْآنَ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَتْ: فَإِنَّ خُلُقَ نَبِيِّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ الْقُرْآنَ.

[صحيح] - [رواه مسلم في جملة حديثٍ طويلٍ]
المزيــد ...

Amesema Sa'd bin Hisham bin Aamiri -alipoingia kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake:
Ewe mama wa waumini, nieleze kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema: Hivi si unasoma Qur'ani? Nikasema: Ndiyo! akasema: Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani.

Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Aliulizwa mama wa waumini Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akajibu kwa neno lilokusanya, na akamuhamisha muulizaji upande wa Qura''ani tukufu iliyo kusanya sifa za ukamilifu, kama alivyosema -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiiga tabia za Qur'ani, iliyoyaamrisha Qur'ani anayaamrisha, na yale inayoyakataza Qur'ani anayaepuka, basi ikawa tabia yake ni kuifanyia kazi Qur'ani, na kusimama katika mipaka yake na kua na adabu na adabu zake kuizingatia Qur'ani na matendo kwa ujumla na mfano wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية القيرقيزية النيبالية اليوروبا الليتوانية الدرية الصومالية الكينياروندا
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika kujipamba kwake na tabia za Qur'ani.
  2. Kusifiwa kwa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, nakuwa tabia hizo zilikuwa zikitoka katika taa ya wahyi.
  3. Qur'ani ndio chimbuko la kila tabia njema.
  4. Tabia katika Uislamu zinakusanya dini yote, kwa kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo.