عَنْ بُسْرِ بْنِ سَعِيدٍ، أَنَّ زَيْدَ بْنَ خَالِدٍ الْجُهَنِيَّ رَضيَ اللهُ عنه، أَرْسَلَهُ إِلَى أَبِي جُهَيْمٍ رَضيَ اللهُ عنه، يَسْأَلُهُ مَاذَا سَمِعَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْمَارِّ بَيْنَ يَدَيِ الْمُصَلِّي؟ قَالَ أَبُو جُهَيْمٍ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَوْ يَعْلَمُ الْمَارُّ بَيْنَ يَدَيِ الْمُصَلِّي مَاذَا عَلَيْهِ لَكَانَ أَنْ يَقِفَ أَرْبَعِينَ خَيْرًا لَهُ مِنْ أَنْ يَمُرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ» قَالَ أَبُو النَّضْرِ: لَا أَدْرِي قَالَ: أَرْبَعِينَ يَوْمًا أَوْ شَهْرًا أَوْ سَنَةً؟
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 507]
المزيــد ...
Kutoka kwa Busru bin Saidi, ya kwamba Zaidi bin Khalidi Al-Juhani, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimtuma kwenda kwa Abuu Juhaim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amuulize alisikia nini kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepita mbele ya anayeswali? Akasema Abuu Juhaim: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Lau angejua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali nini anachokipata, basi kusimama arobaini ni bora kwake kuliko kupita mbele yake" Amesema Abuu Nasri: Sijui alisema: Siku arobaini au miezi au miaka?
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 507]
Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupita mbele ya mwenye kuswali swala ya faradhi au sunna, na kwamba lau angelijua mwenye kufanya hivyo kwa makusudi yale anayoyapata katika madhambi; basi angechagua kusimama arobaini; hilo ni bora zaidi kwake kuliko kupita mbele yake. Amesema Abuu Nasri mpokezi wa hadithi: Sijui alisema: Siku arobaini, au miezi au miaka.