عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدَبٍ وَالْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رضي الله عنهما قَالَا: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ حَدَّثَ عَنِّي بِحَدِيثٍ يُرَى أَنَّهُ كَذِبٌ، فَهُوَ أَحَدُ الْكَاذِبِينَ».
[صحيح] - [رواه مسلم في مقدمته]
المزيــد ...
Kutoka kwa Samura bin Jundab na Mughira bin Shu'ba radhi za Allah ziwe juu yao, wamesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo"
[Sahihi] - - [صحيح مسلم]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayenukuu Hadithi kutoka kwake hali yakuwa anajua au anadhani au dhana yake kubwa kuwa ni kumzulia uongo rehema na amani ziwe juu yake; basi mpokezi atashirikiniana na mwanzilishi wa uongo huu katika dhambi.