عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 3461]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 3461]
Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuifikisha elimu kutoka kwake katika Qur'ani na mafundisho yake (Sunna), hata kama kitu kitakuwa kidogo kama aya moja toka ndani ya Qur'ani au hadithi, kwa sharti mfikishaji awe mjuzi katika kile anachokifikisha na kuwalingania watu kwacho. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna ubaya kusimulia kuhusu wana wa Israeli kwa yale yaliyotokea kwao katika matukio, yale yasiyokinzana na sheria yetu. Kisha akatahadharisha kumzulia uongo, nakuwa yeyote mwenye kumzulia uongo kwa makusudi basi ajiandalie mwenyewe makazi yake motoni.