عن أبي هريرة رضي الله عنه أن أعْرَابيًا أتَى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله، دُلَّنِي على عمل إذا عَمِلتُه، دخلت الجنة. قال: «تَعْبُدُ الله لا تُشرك به شيئا، وتُقِيم الصلاة، وتُؤتي الزكاة المَفْرُوضَة، وتصوم رمضان» قال: والذي نفسي بيده، لا أَزِيْدُ على هذا، فلمَّا ولَّى قال النبي صلى الله عليه وسلم : «من سَرَّه أن يَنْظَر إلى رجُل من أهل الجَنَّة فَلْيَنْظر إلى هذا».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba mtu wa kijijini alimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani" Akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha zaidi ya hapo, basi alipoondoka, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa mtu mmoja katika watu wa vijijini alikuja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ili amjulishe ni jambo gani ambalo akilifanya litamuingiza peponi, akamjibu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kuingia peponi na kusalimika na moto yamesimama mambo haya katika kutimiza nguzo za uislamu, kiasi kwamba alisema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na usimshirikishe na chochote" na ndio maana ya kushuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, ambayo ndiyo nguzo ya kwanza katika nguzo za uislamu, na malengo yake ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada, na hiyo ni kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee, na kuwa usimshirikishe na chochote". "Na usimamishe swala", yaani na usimamishe swala tano alizoziandika Mwenyezi Mungu na akaziwajibisha kwa waja wake kila usiku na mchana, pamoja na hizo ikiwemo na swala ya ijumaa. "Na utimize zaka ya lazima", Yaani utoe zaka ya kisheria ambayo kaiwajibisha Mwenyezi Mungu juu yako, na uipeleke kwa wenye kustahiki. "Na ufunge ramadhani", Yaani udumu na kufunga ramadhani kwa wakati wake. "Akasema, Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake sitozidisha zaidi ya haya" Yaani sitozidisha katika matendo ya wajibu chochote katika haya niliyoyasikia kwako katika mambo ya utiifu. Na akaongeza Imamu Muslim: "Na wala sitopunguza katika hayo". "Pindi alipoondoka akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu", yaani amtazame mtu huyu wa kijijini, kwani huyu ni miongoni mwa watu wa peponi ikiwa atadumu katika kuyafanya yale niliyomuamrisha; kwa kauli yake katika hadithi ya Abuu Ayub -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kama ilivyokuja katika sahihi Muslim "Ikiwa kama atashikamana na haya aliyoamrishwa basi ataingia peponi". Na wala hakutaja katika hadithi hii: Kuhiji nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, pamoja nakuwa ndio nguzo ya tano katika nguzo za uislamu, na huenda lilikuwa tukio hili kabla haijafaradhishwa. Na ukweli wake nikuwa hadithi inaonyesha kuwa atakayetekeleza yale aliyoyafaradhisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa swala tano na kufunga ramadhani na kutoa zaka pamoja na kuyaepuka maharamisho, basi atastahiki kuingia peponi, na kuokoka na moto.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama