+ -

عن عبدِ الله بن عمرو رضي الله عنهما قال:
كنتُ أكتبُ كلَّ شيءٍ أسمعُه من رسولِ الله صلَّى الله عليه وسلم أُريدُ حفْظَه، فنهتْني قريشٌ، وقالوا: أتكْتبُ كلَّ شيءٍ تَسمَعُه من رسول الله صلَّى الله عليه وسلم، ورسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم بَشَرٌ يتكلَّمُ في الغضَبِ والرِّضا؟ فأمسَكتُ عن الكتاب، فذكرتُ ذلك لرسول الله صلَّى الله عليه وسلم، فأومأ بإصبَعِه إلى فيه، فقال: «اكتُبْ، فوالذي نفسي بيدِه، ما يَخرُجُ منه إلا حقٌّ».

[صحيح] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 3646]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kukihifadhi, Makuraishi wakanikataza, na wakasema: Hivi unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu huzungumza wakati wa hasira na furaha? Nikaacha kuandika, nikamueleza hilo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaashiria kwa kidole chake katika kinywa chake, akasema: "Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 3646]

Ufafanuzi

Amesema Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili nikihifadhi kwa kukiandika, mabwana wa kikuraishi wakanikataza, na wakasema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu anazungumza katika furaha na hasira, na huenda akakosea, nikaacha kuandika.
Nikamueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- waliyosema, akaashiria kwa kidole chake kinywani kwake akasema: Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake haitoki ndani yake ila haki kwa hali zote, na katika furaha na hasira.
Na alisema Mtukufu kumuhusu Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hatamki kwa matamanio * Si vinginevyo, ila huo ni wahyi anaofunuliwa" [An najm: 3-4].

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekingwa katika yale anayoyafikisha kutoka kwa Mola wake Aliyetakasika na kutukuka, katika furaha na hasira.
  2. Pupa ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kuihifadhi sunna na kuifikisha.
  3. Kufaa kuapa hata kama hakuna masilahi katika hilo, kama kulitilia mkazo jambo.
  4. Kuiandika elimu ni katika sababu kubwa zinazoihifadhi elimu.