عن عَمْرُو بْنُ عَامِرٍ عَنْ أَنَس بن مالك قَالَ:
كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَوَضَّأُ عِنْدَ كُلِّ صَلَاةٍ، قُلْتُ: كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ؟ قَالَ: يُجْزِئُ أَحَدَنَا الْوُضُوءُ مَا لَمْ يُحْدِثْ.
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 214]
المزيــد ...
Kutoka kwa Amri bin Aamiri kutoka kwa Anasi amesema:
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala, nikasema: Nyinyi mlikuwa mnafanya vipi? Akasema: Ulikuwa ukimtosha mmoja wetu udhu mmoja madam hajatengukwa.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 214]
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kwa kila swala ya faradhi hata kama hajatengukwa udhu; Na hii ni kwa sababu ya kupata malipo na fadhila.
Na inafaa kwa mtu kuswali kwa zaidi ya swala moja kwa udhu mmoja madam bado yuko na udhu wake.