عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إذا توضَّأ أحدُكُم فَليَجعَل في أنفِه ماءً، ثم ليَنتَنْثِر، ومن اسْتَجمَر فَليُوتِر، وإذا اسْتَيقَظَ أَحَدُكُم من نومِه فَليَغسِل يَدَيه قبل أن يُدْخِلهُما في الإِنَاء ثلاثًا، فإِنَّ أَحدَكُم لا يَدرِي أين بَاتَت يده». وفي رواية: «فَليَستَنشِق بِمِنْخَرَيه من الماء». وفي لفظ: «من توضَّأ فَليَسْتَنشِق».
[صحيح] - [الرواية الأولى: متفق عليها. الرواية الثانية: رواها مسلم. الرواية الثالثة: متفق عليها، ولفظ مسلم: (فليستنثر)، بدل: (فليستنشق)]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke puani mwake maji, kisha apenge, na atakayestanji kwa mawe basi ayafanye kuwa witiri, na atakapoamka mmoja wenu toka usingizini mwake basi na aoshe mikono yake kabla hajaiingiza katika chombo mara tatu, kwani hakika mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na katika riwaya nyingine: "Basi na apandishe katika tundu zake za pua maji". Na katika tamko jingine: "Atakayetawadha basi na apandishe maji puani".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Inakusanya hadithi hii vipengele vitatu: kila kipengele kina hukumu yake maalumu: 1. Ametaja kuwa mwenye kutawadha atakapoanza kutawadha aingize maji puani mwake, kisha ayatoe, nako ni kupandisha maji na kuyapenga kuliko tajwa katika hadithi; kwasababu pua ni katika uso ambao ameamrishwa mwenye kutawadha auoshe, na zimemiminika hadithi sahihi juu ya sheria ya hilo; kwasababu ni katika usafi unaotakiwa kisheria. 2. Kisha akataja kuwa atakayetaka kuondoa uchafu uliotoka kwake kwa kutumia mawe, basi kuwe kuundoa huo uchafu ni kwa witiri, chini kabisa ni tatu na juu zaidi ni kile kitakachoweza kuuondoa uchafu uliotoka, na kitasafisha mahali kikiwa idadi ya witiri, na kama hakitosafisha basi azidishe moja, itakayoleta witiri kutoka katika shufa (namba inayogawanyika). 3. Na akataja pia kuwa mwenye kuamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize viganja vyake katika chombo, au kushika kitu kibichi, mpaka avioshe mara tatu, kwasababu usingizi wa usiku mara nyingi unakuwa mrefu, na mkono wake unazunguka katika mwili wake, huenda ukapatwa na baadhi ya vitu vichafu haliyakuwa yeye hajui, ikawekwa sheria kwake kuuosha kwaajili ya usafi wa kisheria.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama