عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«سَوُّوا صُفُوفَكُمْ، فَإِنَّ تَسْوِيَةَ الصَّفِّ مِنْ تَمَامِ الصَّلَاةِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 433]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake:
"Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 433]
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kuswali kunyoosha safu zao, na wasitanguliane wala wasirudi nyuma, na kwamba kuzinyoosha ni sehemu ya kukamilisha na ukamilifu wa Sala, na kuwa kupinda kwa safu ni dosari na ni upungufu ndani yake.