عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«أَمَا يَخْشَى أَحَدُكُمْ - أَوْ: لاَ يَخْشَى أَحَدُكُمْ - إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ قَبْلَ الإِمَامِ، أَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ رَأْسَهُ رَأْسَ حِمَارٍ، أَوْ يَجْعَلَ اللَّهُ صُورَتَهُ صُورَةَ حِمَارٍ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 691]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 691]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kuwa Mwenyezi Mungu kukifanya kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda.