عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يَزِيدَ الخَطْمِيِّ قَالَ: حَدَّثَنِي البَرَاءُ وَهُوَ غَيْرُ كَذُوبٍ، قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَالَ: سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، لَمْ يَحْنِ أَحَدٌ مِنَّا ظَهْرَهُ حَتَّى يَقَعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَاجِدًا، ثُمَّ نَقَعُ سُجُودًا بَعْدَهُ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 690]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Yazidi Al-Khatmiy amesema: Alinisimulia Al-Baraa naye si mtu wa kukadhibishwa, akasema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 690]
Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Allah ziwe juu yake naye ni mkweli, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anasema: Sami'allahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi), walikuwa wakiendelea kusimama walioko nyuma yake, na hainamishi yeyote miongoni mwao mgongo wake kwa ajili ya kusujudu mpaka aweke rehema na amani ziwe juu yake paji lake la uso katika Ardhi, kisha wanaporomoka wote kwa kusujudu baada yake.