عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«أَطْعِمُوا الجَائِعَ، وَعُودُوا المَرِيضَ، وَفُكُّوا العَانِيَ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 5373]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 5373]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika haki za Muislamu kwa ndugu yake Muislamu ni kumlisha mwenye njaa na kumtembelea mgonjwa, na kumuacha huru mateka.