Aina:
+ -

عَنِ النَّوَّاسِ بْنِ سِمْعَانَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«البِرُّ: حُسْنُ الخُلُقِ، وَالإِثْمُ مَا حَاكَ فِي صَدْرِكَ، وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ». وَعَنْ وَابِصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «جِئْتَ تَسْأَلُ عَنِ البِرِّ وَالإِثْمِ»، قُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: «اسْتَفْتِ قَلْبَكَ، البِرُّ: مَا اطْمَأَنَّتْ إلَيْهِ النَّفْسُ، وَاطْمَأَنَّ إلَيْهِ القَلْبُ، وَالإِثْمُ: مَا حَاكَ فِي نَفْسِكَ وَتَرَدَّدَ فِي الصَّدْرِ، وَإِنْ أَفْتَاكَ النَّاسُ وَأَفْتَوْكَ».

[صحيح] - [الحديث الأول: رواه مسلم، والحديث الثاني: رواه أحمد والدارمي.] - [الأربعون النووية: 27]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile lililokukereketa katika nafsi yako na ukawa hukupendezwa watu walione".

[Sahihi] - [الحديث الأول: رواه مسلم، والحديث الثاني: رواه أحمد والدارمي] - [الأربعون النووية - 27]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na uovu, akasema: Hakika jambo kubwa zaidi katika wema ni tabia njema pamoja na Mwenyezi Mungu kwa kumuogopa, na pamoja na viumbe kwa kustahamili maudhi yao, na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na kuunga udugu na utiifu na upole na kuwapa watu udhuru na kuishi nao vizuri na ujamaa mzuri. Nakuwa wema ni ule uliotulizana kwao moyo na nafsi. Na ama dhambi ni katika lile ambalo nafsi itataharuki kutokana na mambo yenye utata na ikapata shaka pasina kukunjuka kifua, na moyo ukapatwa na shaka, na ukaogopa kwakuwa ni dhambi, ukawa haukutaka kulidhihirisha kwakuwa ni jambo baya kwa mtu na kwa watu wengine pia, na hii ni kwa sababu tabia ya nafsi hupenda kutazamwa na watu wengine ikifanya kheri; na hata kama watu watakupa majibu mazuri usichukue majibu yao madamu alama za utata zinazunguka ndani ya nafsi yako majibu yao hayawezi kuondoa utata madamu utata ni wa kweli na akawa anayekupa majibu anatoa pasina elimu; ama ikiwa majibu yanatokana na dalili ya kisheria kilichowajibu kwa mpewa majibu arejee katika hilo, hata kama moyo wake hautokunjuka kwa hilo.

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuwa na tabia njema; kwa sababu tabia njema ni katika mambo makubwa ya wema.
  2. Haki na batili haviwezi kumchanganya muumini, bali anaijua haki kwa nuru aliyonayo ndani ya moyo wake, na anaichukia batili na kuikataa.
  3. Miongoni mwa alama za dhambi ni moyo kukosa utulivu na kuwa na shaka, na kuchukia watu wasilione.
  4. Amesema As-Sanadi: Hii ni katika mambo yenye kutatiza ambayo watu hawajui kutofautisha moja kati ya pande mbili; na kama si hivyo basi kilichoamrishwa na sheria pasina kuonekana dalili ndani yake ni kinyume na hilo katika wema, na yaliyokatazwa hivyo hivyo miongoni mwa madhambi, na hayo hakuna haja ya kuuliza ama kuutazama moyo na kuona utulivu wake.
  5. Wanaosemeshwa katika hadithi hii ni wale wenye maumbile salama (ambao mioyo yao na akili zao hazijavurugwa na fikra potofu), na si wenye mioyo iliyofunikwa isiyojua jema wala kulikataa ovu isipokuwa yale iliyonyweshwa katika matamanio yake.
  6. Amesema Attwayibi: Inasemekana: Imefasiriwa maana ya wema katika hadithi kwa maana nyingi, akaifasiri katika baadhi ya sehemu kuwa ni yale ambayo nafsi imetulizana kwayo na moyo ukatuliza pia, na akaifasiri katika sehemu nyingine kuwa ni imani, na katika sehemu nyingine, kwa yale yanayokuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na hapa ameifasiri kwa kuwa na tabia njema, na akafasiri tabia njema kuwa: Ni kuvumilia maudhi na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na yote hayo yanakaribiana katika maana.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai German Pashto Kiassam Albanian الأمهرية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga المجرية التشيكية الموري Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية الخميرية
Kuonyesha Tarjama
Aina tofauti
Ziada