عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَوْ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَوَكَّلُونَ عَلَى اللهِ حَقَّ تَوَكُّلِهِ لَرَزَقَكُمْ كَمَا يَرْزَقُ الطَّيْرَ تَغْدُو خِمَاصًا وَتَرُوحُ بِطَانًا».
[صحيح] - [رواه الإمام أحمد، والترمذي، والنسائي، وابن ماجه، وابن حبان في صحيحه، والحاكم] - [الأربعون النووية: 49]
المزيــد ...
Kutoka kwa Omari bin Khatwab radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Laiti nyinyi mgetegemea kwa Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, wanarudi jioni wakiwa wameshiba".
[Sahihi] - [رواه الإمام أحمد والترمذي والنسائي وابن ماجه وابن حبان في صحيحه والحاكم] - [الأربعون النووية - 49]
Anatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.