عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما قال: قال رَسولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا، وَإِنْ كَانَتْ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ فِيهِ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا: مَنْ إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وإذَا خَاصَمَ فَجَرَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ».
[صحيح] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية: 48]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mambo manne yatakayekuwa kwake basi atakuwa mnafiki, ana akiwa na jambo moja miongoni mwa hayo basi atakuwa na tabia ya unafiki mpaka aiache: Yule anayesimulia akasema uongo, na akiahidi hatimizi, na akigombana hupita mipaka, na akiingia makubaliano hufanya hiyana".
[Sahihi] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية - 48]
Tabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni:
Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake.
Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye.
Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume.
Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo.
Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.