عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ أَبِي مُوسَى الأَشْعَريِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَهُ إِلَى اليَمَنِ، فَسَأَلَهُ عَنْ أَشْرِبَةٍ تُصْنَعُ بِهَا، فَقَالَ: وَمَا هِيَ؟، قَالَ: «البِتْعُ وَالمِزْرُ»، فَقِيلَ لِأَبِي بُرْدَةَ: مَا البِتْعُ؟ قَالَ: نَبِيذُ العَسَلِ، وَالمِزْرُ: نَبِيذُ الشَّعِيرِ، فَقَالَ: «كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ» خرجه البخاري.
وَخَرَّجَهُ مُسْلِمٌ وَلَفْظُهُ: قَالَ: بَعَثَنِي رَسُولُ اَلله أَنَا وَمُعَاذٌ إِلَى اَليَمَنِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولُ اَللَّهِ! إِنَّ شَرَابًا يُصْنَعُ بِأَرْضِنَا يُقَال لَهُ: المِزَرُ مِنَ الشَّعِيرِ، وَشَرَابٌ يُقَالُ لَهُ: البِتْعُ مِنَ العَسَلِ، فَقَالَ: «كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ».
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: «فَقَالَ: كُلُّ مَا أَسْكَرَ عَنِ الصَّلَاةِ فَهُوَ حَرَامٌ».
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ: «وَكَانَ رَسُولُ الله قَدْ أُعْطِيَ جَوَامِعَ الكَلِمِ بِخَوَاتِمِهِ، فَقَالَ: أَنْهَى عَنْ كُلِّ مُسْكِرٍ أَسْكَرَ عَنْ الصَّلَاةِ».
[صحيح] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية: 46]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Buraida, kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abuu Musa A-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji fulani vinavyotengenezwa huko, akasema: Ni vipi hivyo?, akasema: "Ni Bit'u na Mizru" akaulizwa Abuu Buraida: Bit'u ni nini? Akasema: Ni mvinyo wa Asali, na Mizru: Ni mvinyo wa ngano, akasema: "Kila kilevi ni haramu" Ameitoa Bukhari.
-
Anaeleza Abuu Musa Al-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyo tengenezwa huko je ni haramu, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo. Akasema Abuu Musa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ni Bit'u: Yaani mvinyo wa Asali, na Muruuz: Ni mvinyo wa ngano. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na alikuwa amepewa maneno machache yenye maana pana: "Kile chenye lewesha ni haramu".