____
[] - []
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Hamza Anas bin Maaliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake mtumishi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [الأربعون النووية - 13]
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, katika matendo mema, na aina mbalimbali za wema katika dini na dunia, na achukie kwake kinachochukiwa na nafsi yake, na ikiwa ataona kwa ndugu yake Muislamu kuna upungufu katika dini yake, basi ajitahidi kurekebisha, na akiona kuna jambo la kheri basi amtie moyo na amsaidie, na amnasihi katika dini yake au mambo ya dunia yake.