عَنْ أَبِي مُـحَمَّدٍ الحَسَنِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ - سِبْطِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَيْحَانَتِهِ-، قَالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«دَعْ مَا يَرِيبُك إلَى مَا لَا يَرِيبُكَ».
[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي] - [الأربعون النووية: 11]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Muhammadi Al-Hasan bin Ally bin Abii Twalib mjukuu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na marashi yake (kipenzi chake), amesema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka."
-
Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha lile linalokutia shaka ndani yake katika kauli na matendo kuwa limekatazwa au la, je ni halali au ni haramu, na ufanye yale usiyo na shaka nayo katika yale uliyo na uhakika na uzuri wake na uhalali wake.