عَنْ أَبِي أُمَامَةَ البَاهِلِيِّ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: ذُكِرَ لِرَسُولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلاَنِ أَحَدُهُمَا عَابِدٌ وَالآخَرُ عَالِمٌ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«فَضْلُ العَالِمِ عَلَى العَابِدِ كَفَضْلِي عَلَى أَدْنَاكُمْ»، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَأَهْلَ السَّمَوَاتِ وَالأَرَضِينَ حَتَّى النَّمْلَةَ فِي جُحْرِهَا وَحَتَّى الحُوتَ لَيُصَلُّونَ عَلَى مُعَلِّمِ النَّاسِ الخَيْرَ».
[حسن لغيره] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2685]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Umama Al-Baahili radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Walitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu wawili, mmoja wao mchamungu na mwingine msomi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu", Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake na wakazi wa mbinguni na ardhini hata mdudu chungu katika shimo lake na hata samaki humtakia rehema mwenye kuwafundisha watu mambo ya kheri".
[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 2685]
Walitajwa watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mmoja wao ni mchamungu, na mwingine msomi, ni yupo mbora kati yao?
Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ubora wa msomi wa elimu ya kisheria mwenye kuifanyia kazi na mwenye kuifundisha kwa mchamungu aliyejitenga kwa ajili ya ibada, pamoja na kujua kwake yale ya wajibu kwake katika elimu ni kama ubora wake rehema na amani ziwe juu yake na utukufu wake kwa Swahaba wa chini zaidi. Kisha akabainisha rehema na amani ziwe juu yake sababu ya hilo, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika wake miongoni mwa wabeba Arshi, na wakazi wa mbinguni katika Malaika wengineo, na wakazi wa Ardhi kwanzia binadam na majini na wanyama wote, hata mdudu chungu katika makazi yake ndani ya tumbo la Ardhi, na hata nyangumi na samaki wa Baharini; alitaja hivi ili waingie katika kauli hii viumbe wa nchi kavu na Baharini, wote hawa wanamuombea mazuri mwenye kuwafundisha watu elimu ya dini ambayo ndani yake kuna uokovu wa watu na mafanikio yao.