+ -

عَنْ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ قَالَ: سَمِعْتُ عُثْمَانَ ابْنِ عَفَّانَ رضي الله عنه يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَنْ قَالَ بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ، فِي الْأَرْضِ، وَلَا فِي السَّمَاءِ، وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ، ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، لَمْ تُصِبْهُ فَجْأَةُ بَلَاءٍ، حَتَّى يُصْبِحَ، وَمَنْ قَالَهَا حِينَ يُصْبِحُ ثَلَاثُ مَرَّاتٍ، لَمْ تُصِبْهُ فَجْأَةُ بَلَاءٍ حَتَّى يُمْسِيَ»، قَالَ: فَأَصَابَ أَبَانَ بْنَ عُثْمَانَ الْفَالِجُ، فَجَعَلَ الرَّجُلُ الَّذِي سَمِعَ مِنْهُ الْحَدِيثَ يَنْظُرُ إِلَيْهِ، فَقَالَ لَهُ: مَا لَكَ تَنْظُرُ إِلَيَّ؟ فَوَاللَّهِ مَا كَذَبْتُ عَلَى عُثْمَانَ، وَلَا كَذَبَ عُثْمَانُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَلَكِنَّ الْيَوْمَ الَّذِي أَصَابَنِي فِيهِ مَا أَصَابَنِي غَضِبْتُ فَنَسِيتُ أَنْ أَقُولَهَا.

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه والنسائي في الكبرى وأحمد] - [سنن أبي داود: 5088]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abana bin Othman amesema: Nilimsikia Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake akisema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 5088]

Ufafanuzi

Ameainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema asubuhi ya kila siku baada ya kuchomoza Alfajiri, na jioni ya kila usiku kabla ya kuzama jua mara tatu: "Bismillaah" Ninataka msaada na ninajilinda dhidi ya kila chenye kuudhi "ambaye hakidhuru" kwa kulitaja "pamoja na jina lake" yaani "chochote" vyovyote vile kitakavyokuwa kikubwa "katika ardhi" na vinavyotoka ndani yake miongoni mwa mabalaa "wala mbinguni" na kinachoshuka kutoka humo miongoni mwa mabalaa "naye ni msikivu" wa kauli zetu "mjuzi" wa hali zetu.
..... Atakayesema wakati wa jioni halitomfika balaa la ghafla mpaka afike asubuhi, na atakayesema wakati wa asubuhi balaa halitomfika la ghafla mpaka afike jioni.
Akaipatia riwaya ya hadithi ya Abana bin Othman Al-Falij; Nayo ni kudhoofika kwa baadhi ya upande wa mwili, yule bwana aliyesikia kwake hadithi akamtazama Abana kwa kustaajabu?! Abana akasema kumwambia yule bwana: Mbona wanitazama?! Wallah sijamzulia uongo Othman, wala Othman hajamzulia uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini leo yamenifika yale aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwangu kuyasema, nimepatwa na hasira nikasahau kusema maneno haya yaliyotajwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inapendeza kuleta dhikri hii asubuhi na jioni; ili mwanadam ahifadhike kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu lisimfike balaa ghafla au madhara ya msiba au mfano wa hayo.
  2. Nguvu kubwa ya yakini kwa wema wa mwanzo kwa Mwenyezi Mungu na kuyasadikisha kwao yale aliyoyaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Miongoni mwa faida za kufanywa dhikri ziwe za asubuhi na ajioni ni kuondoa hali ya kughafilika kwa muislamu na kuvuta kwake picha endelevu kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Kwa kadiri inavyokuwa imani ya mtajaji Mwenyezi Mungu na unyenyekevu wake na kuhudhurisha kwake moyo, pamoja na kutakasa nia na yakini ndivyo itakavyozidi kupatikana athari ya dhikri.