+ -

عَنْ وَابِصَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأَى رَجُلًا صَلَّى وَحْدَهُ خَلْفَ الصَّفِّ، فَأَمَرَهُ أَنْ يُعِيدَ صَلَاتَهُ.

[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [مسند أحمد: 18000]
المزيــد ...

Kutoka kwa Waabiswa radhi za Allah ziwe juu yake:
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.

[Ni nzuri] - - [مسند أحمد - 18000]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja aliyeswali nyuma ya safu peke yake, akamuamrisha arudie swala yake; kwa sababu swala yake haikusihi kwa hali hii.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuwahi swala ya jamaa na kuwahi mbele kwa ajili yake, na asiswali nyuma ya safu peke yake ili swala yake asiitie katika kubatilika
  2. Amesema bin Hajari: Atakayeanza swala peke yake nyuma ya safu kisha akaingia katika safu kabla ya kunyanyuka kutoka katika rukuu, hatolazimika kurudia, kama ilivyokuja katika hadithi ya Abiibakra, na vinginevyo itakuwa wajibu kwa mujibu wa ujumla wa hadithi ya Waabiswa.