+ -

عن علي بن أبي طالب، ومعاذ بن جبل رضي الله عنهما مرفوعًا: «إذا أتى أحدُكم الصلاةَ والإمامُ على حال، فلْيصنعْ كما يصنع الإمامُ».
[صحيح] - [رواه الترمذي]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ally bin Abii Twalib, na Mua'dh bin Jabali- radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya imamu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

Ufafanuzi

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, ima ya kusimama au kurukuu au kusujudu au kukaa, basi aendane na imamu pale alipo katika kusimama au kurukuu au kitendo kinginecho, na asisubiri mpaka anyanyuke imamu kama wanavyofanya baadhi ya watu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kuingia mwenye kuungana pamoja na imamu katika kipengele chochote miongoni mwa vipengele vya swala atakachokikuta, bila kutofautisha kati ya rukuu na sijida na kukaa.
  2. Nikuwa kuipata rakaa ambayo ameungana na imamu kunakuwa kwa kuikuta rukuu yake, kama zilivyoonyesha juu ya hilo dalili zingine.