عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: علمنا رسول الله صلى الله عليه وسلم خطبة الحاجة: إن الحمد لله، نستعينه ونستغفره، ونعوذ به من شرور أنفسنا، من يهد الله، فلا مضل له، ومن يضلل، فلا هادي له، وأشهد أن لا إله إلا الله، وأشهد أن محمدا عبده ورسوله، " يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ والأرحام إن الله كان عليكم رقيبا} [النساء: 1] ، {يا أيها الذين آمنوا اتقوا الله حق تقاته ولا تموتن إلا وأنتم مسلمون} [آل عمران: 102] ، {يا أيها الذين آمنوا اتقوا الله وقولوا قولا سديدا (70) يصلح لكم أعمالكم ويغفر لكم ذنوبكم ومن يطع الله ورسوله فقد فاز فوزا عظيما} [الأحزاب:70 - 71].
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه والنسائي وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Alitufundisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Hotuba ya haja: Hakika kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, tunamtaka msaada na tunamuomba msamaha, na tunajilinda kwake kutokana na shari ya nafsi zetu, mwenye kumuongoza Mwenyezi Mungu, hakuna wa kumpoteza, ana anayempoteza, hakuna wa kumuongoza, na nina shuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, "Enyi watu, mcheni Mola wenu aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akaumba kutokana na nafsi hiyo mwanamke, na akatoa kutokana na nafsi hiyo wanaume na wanawake wengi, na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mnaombana na jamaa zenu, hakika Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mlinzi" [An nisaa: 1], "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu ukweli wa kumcha na wala msife ila na nyinyi ni waislamu" [Al Imran: 102], "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na mseme kauli ya sawa [70] akutengenezeeni amali zenu na akusameheni madhambi yenu na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi atakuwa kafaulu kufaulu kukubwa" [Al Ahzaab: 70-71].
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Imeonyesha hadithi ya bin Mas'udi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, juu ya sheria ya hotuba hii iliyokusanya sifa nyingi za Mwenyezi Mungu, na kutaka msaada wake, na kujilinda kwake kutokana na shari, na kusoma aya zile tukufu, na inampasa mtu azitangulize mbele wakati wa kuzungumza na watu katika elimu, hiyo ni katika mafundisho ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna, na utambuzi wa sheria, na mawaidha kwa watu, haihusu ndoa pekee, bali ni hotuba ya kila haja; ili ziteremke baraka, na kuwe na athari nzuri katika yale unayoyatoa, hiyo ni sunna iliyotiliwa mkazo.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto
Kuonyesha Tarjama

من فوائد الحديث

  1. Nikuwa haja yoyote ni sunna kuifungua kwa hotuba hii, kwani itafaulu kwa baraka za dhikiri hii.
  2. Nikuwa hotuba lazima iwe imekusanya shukurani, na shahada mbili, na baadhi ya aya za Qur'ani.
  3. Hadithi hii ndiyo hotuba, huitwa hotuba ya haja, na ni sunna katika kuzungumza na watu mambo ya kielimu kuchukua katika mafundisho ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna, na utambuzi wa sheria, na kuwapa mawaidha watu, hii haihusu ndoa pekee, bali ni hotuba ya kila haja, na ndoa ni miongoni mwa haja hizo.
  4. Hadithi imekusanya juu ya sifa za mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu, na kustahiki kwake sifa hizo, na kusifika kwake na sifa hizo.
  5. Hadithi imekusanya kutaka msaada kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu-, na msaada wa kutaka kufanyiwa wepesi, na wepesi katika haja ambayo ataielekea mtu, hasa hasa ndoa kwa gharama zake na matumizi yake.
  6. Hadithi imekusanya juu ya kutaka msamaha kutoka kwake -Mtukufu- na stara ya aibu na madhambi, na kukiri mapungufu na uzembe, na ayafute hayo na ayasamehe.
  7. Hadithi imekusanya juu ya kutaka ulinzi kwake, na kushikamana naye, kutokana na shari za nafsi yenye kuamrisha maovu, ambayo inamvuta katika kufanya mambo ya haramu, na kuacha ya wajibu,ispokuwa aliyekingwa na Mwenyezi Mungu na akamlinda.
  8. Hadithi imekusanya juu ya kukiri kuwa yeye Mtukufu ndiye mwenye maamuzi ya moja kwa moja kwa viumbe wake, nakuwa uongofu wa nyoyo na upotofu wake uko mkononi mwake.
  9. Hadithi imekusanya juu ya kukiri shahada mbili ambazo ndiyo ufunguo wa uislamu, na ndizo asili yake na msingi wake, kwasababu mtu hawezi kuwa muislamu ila kwa kuzikubali, kwa kukiri kuliko chimbuka toka moyoni mwake.