عن أبي موسى رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«لا نِكَاحَ إِلّا بِوَليٍّ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 2085]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
"Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad] - [Sunanu Abii Daud - 2085]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwanamke haikubaliki ndoa yake ila kwa walii atakayesimamia kufungwa kwa ndoa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Walii ni sharti la kusihi ndoa, ikifanyika bila walii, au mwanamke akajiozesha mwenyewe, haikubaliki.
  2. Walii ni ndugu wa karibu wa kiume kwa mwanamke, asiozeshwe na walii wa mbali akiwepo walii wa karibu yake.
  3. Ni sharti kwa walii: Awe mtu mzima (Aliyebalehe), mwanaume, na uwezo wa kupambanua na kujua masilahi ya ndoa, na wawe katika dini moja, msimamizi na msimamiwa, asiyekuwa na sifa hizi hastahiki kuwa msimamizi wa kufungisha ndoa.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (58)