+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي لله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً، إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ» أَوْ قَالَ: «غَيْرَهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1469]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine" Au alisema: "Tabia tofauti na hiyo"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1469]

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mume kumchukia sana mke wake hadi kupelekea dhulma, na kumuacha na kumtelekeza; Mwanadamu ana asili ya kutokamilika, na ikiwa atachukia kwake tabia moja mbaya, basi atapata tabia nyingine nzuri; ataridhia kwa tabia hiyo nzuri anayoikubali, na avumilie kwa tabia asizozipenda miongoni mwa tabia mbaya, ambazo humfanya awe mvumilivu na asimchukie kiasi cha kutaka kumuacha.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Huu ni wito kwa muumini wa kuja katika haki na uadilifu, na kuhukumu mambo kwa akili katika mgogoro wowote unaotokea baina yake na mke wake, na sio kutoa maamuzi kwa hisia na mihemuko ya muda mfupi.
  2. Kazi ya muumini si kumchukia mwanamke muumini kabisa mpaka afikie kuachana naye, bali apuuze kile anachochukia kwa kile anachopenda.
  3. Himizo la kuishi vizuri na kutengeneza urafiki kati ya wanandoa.
  4. Imani ni msukumo wa maadili mema, hivyo hakuna muumini wa kiume au wa kike asiye na tabia njema; Imani inachochea uwepo wa sifa njema ndani yao.