Aina:

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما مرفوعاً: «الدنيا متاع، وخير متاعها المرأة الصالحة».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Amriy bin Aaswi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Dunia kwa yale yaliyomo ni kitu cha kustarehesha kwa muda kisha kinatoweka, lakini starehe bora ya hii dunia yenye kuondoka ni mke mwema, anayesaidia kuipata Akhera, na amefafanua Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kwa kauli yake kuwa: "Akimtazama anamfurahisha, na akimuamrisha anamtii, na akiwa mbali naye anamuhifadhi katika nafsi yake na mali yake".

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inafaa kustarehe na mazuri ya dunia ambayo ameyahalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kupita kiasi wala kujifaharisha.
  2. Kuhamasishwa katika kuchagua mke mwema kwasababu yeye ni msaada kwa mwanaume katika kumtii Mola wake.
  3. Starehe bora ya dunia ni ile inayokuwa katika utiifu wa Mwenyezi Mungu au inayosaidia katika hilo.
Aina tofauti
Ziada