عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا، وَخَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِنِسَائِهِمْ».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 1162]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 1162]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba mtu aliyekamilika zaidi kiimani ni yule itakayekuwa nzuri tabia yake, na hii kwa kuwa na uso mkunjufu, na kutenda mema, na maneno mazuri, na kuacha maudhi.
Na muumini bora kuliko wote ni yule mbora kwa wake zake, kama mke wake na mabinti zake na dada zake na ndugu zake wengine wa kike; kwa sababu wao ndio watu wenye haki zaidi kutendewa tabia nzuri.