عَنْ أَبِي حُمَيْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
اسْتَعْمَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا عَلَى صَدَقَاتِ بَنِي سُلَيْمٍ، يُدْعَى ابْنَ اللُّتْبِيَّةِ، فَلَمَّا جَاءَ حَاسَبَهُ، قَالَ: هَذَا مَالُكُمْ وَهَذَا هَدِيَّةٌ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَهَلَّا جَلَسْتَ فِي بَيْتِ أَبِيكَ وَأُمِّكَ، حَتَّى تَأْتِيَكَ هَدِيَّتُكَ إِنْ كُنْتَ صَادِقًا» ثُمَّ خَطَبَنَا، فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَمَّا بَعْدُ، فَإِنِّي أَسْتَعْمِلُ الرَّجُلَ مِنْكُمْ عَلَى العَمَلِ مِمَّا وَلَّانِي اللَّهُ، فَيَأْتِي فَيَقُولُ: هَذَا مَالُكُمْ وَهَذَا هَدِيَّةٌ أُهْدِيَتْ لِي، أَفَلاَ جَلَسَ فِي بَيْتِ أَبِيهِ وَأُمِّهِ حَتَّى تَأْتِيَهُ هَدِيَّتُهُ، وَاللَّهِ لاَ يَأْخُذُ أَحَدٌ مِنْكُمْ شَيْئًا بِغَيْرِ حَقِّهِ إِلَّا لَقِيَ اللَّهَ يَحْمِلُهُ يَوْمَ القِيَامَةِ، فَلَأَعْرِفَنَّ أَحَدًا مِنْكُمْ لَقِيَ اللَّهَ يَحْمِلُ بَعِيرًا لَهُ رُغَاءٌ، أَوْ بَقَرَةً لَهَا خُوَارٌ، أَوْ شَاةً تَيْعَرُ» ثُمَّ رَفَعَ يَدَهُ حَتَّى رُئِيَ بَيَاضُ إِبْطِهِ، يَقُولُ: «اللَّهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ» بَصْرَ عَيْنِي وَسَمْعَ أُذُنِي.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6979]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Humaid Assaaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6979]
Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja akiitwa: Bin Lutbia ya kukusanya Zaka kutoka katika kabila la Bani Suleim, aliporejea Madina akampa mahesabu ya mali aliyokusanya na aliyotumia, akasema bin Lutbia: Hii ndio mali yenu niliyoikusanya kutoka katika Zaka, na mali hii nimepewa zawadi mimi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake kumwambia: Hivi si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako ili uone je utapewa zawadi ikiwa wewe ni mkweli; kwani hakika haki ulizozifanyia kazi ndio sababu ya kupewa kwako zawadi, na kwamba lau ungekaa nyumbani kwako usingezawadiwa chochote, hupaswi kuihalalisha kwakuwa tu imekufikia kwa njia ya zawadi. Kisha akapanda Mimbari rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya kuhutubia huku akiwa na hasira, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni kama mfanya kazi na muajiriwa katika kile ambacho Mwenyezi Mungu kanipa maamuzi ndani yake miongoni mwa Zaka na Ngawira, kisha anakuja kutoka katika kazi yake na anasema: Hii ni yenu na hii ni zawadi yangu nimezawadiwa! Kwa nini asikae nyumbani kwa baba yake na mama yake ili zawadi yake imfuate, Wallah, namuapa Mwenyezi Mungu, hatochukua yeyote chochote katika vile anavyopewa isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kakibeba siku ya Kiyama juu ya shingo yake, ikiwa alichokichukua ni Ngamia mwenye sauti, au Ng'ombe mwenye sauti ya mroromo, au mbuzi mwenye mlio, basi atapiga kelele. Kisha akanyanyua mikono yake kwa kasi mpaka waliokaa wakaona weupe wa kwapa lake, kisha akasema: Shuhudieni kuwa nimefikisha hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenu. Kisha Abuu Humaidi Assaaidi akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Kuwa haya ni miongoni mwa mambo ambayo macho yake yaliyashuhudia na masikio yake yakayasikia.