عن ابن مسعود رضي الله عنه مرفوعًا: «إِنَّها سَتَكُون بَعدِي أَثَرَة وأُمُور تُنكِرُونَها!» قالوا: يا رسول الله، فَمَا تَأمُرُنَا؟ قال: «تُؤَدُّون الحَقَّ الذي عَلَيكم، وتَسأَلُون الله الذِي لَكُم».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika ukweli ni kwamba utakuja kutokea uchoyo baada yangu na mambo msiyoyajua(uzushi)!" wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki iliyo juu yenu, na mumuombe Mwenyezi Mungu haki yenu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Katika hadithi kuna tahadhari juu ya jambo kubwa linalohusiana na mambo ya watawala, nalo ni dhulma ya watawala kwa kujipendelea kwao mali ya umma pasi na kuwajali raia wao, kiasi kwamba ameeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa watakuja kuwatawala waislamu viongozi wanaojipendelea mali za waislamu, wanazitumia watakavyo na wanawazuia waislamu haki yaokatika hiyo mali. Na huu ni uchoyo na dhulma kutoka kwa viongozi hawa, kujipendelea wao mali za waislamu ambazo wao wana haki, na wajipendelee wao nafsi zao na kuwanyima waislamu, lakini maswahaba walioridhiwa walitaka kupata maelekezo ya kiutume katika matendo yao si kwa yale yanayowahusu viongozi, wakasema: Unatuamrisha nini? Na hili linaonyesha ukomavu wa akili zao, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Mtekeleze haki iliyo juu yenu" Yaani kusiwazuieni kule kujipendelea kwao mali juu yenu mkajizuia kuyafanya yale ya wajibu kwenu upande wao, kama kusikiliza na kutii na kutoamsha hisia na kuanzisha fitina (vurugu) bali subirini na msikilize na mtii, na wala msizozane juu ya madaraka aliyowapa Mwenyezi Mungu, "Na mumuombe Mwenyezi Mungu haki yenu" Yaani ombeni haki ambayo ni ya kwenu toka kwa Mwenyezi Mungu, Yaani: Muombeni Mwenyezi Mungu awaongoze hao mpaka watimize haki ambayo iko kwao kwenu nyinyi, na hii ni katika hekima za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-; kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- alijua kuwa nafsi huwa haziwezi kusubiri katika haki yake, nakuwa haziwezi kuridhika juu ya yule anayejipendelea juu yake katika haki zao, lakini yeye -Rehema na Amani akaelekeza katika jambo ambalo ndani yake lina kheri na maslahi, na zinatoweka nyuma yake shari nyingi na fitina nyingi, nalo ni sisi tutimize haki zilizo juu yetu kwao kama kusikia na kutii na kutozozana juu ya uongozi na mfano wa hayo, na tumuombe Mwenyezi Mungu haki yetu.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama